Abstract:
Suala la athari katika uhawilishaji wa kwenye ujumbe wa lugha chanzi katika tafsiri si geni. Tafiti nyingi zimelishughulikia suala hili lakini tafiti hizo zimeegemea sana katika athari ya uhawilishaji wa ujumbe kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza athari ya uhawilishaji wa kwa ujumbe wa lugha chanzi katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2019). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1989) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Natharia hizi zilisaidia kuchuguza athari ya uhawilishaji wa kwa ujumbe asilia katika vitabu teule. Data ya utafiti huu ilipatikana kwa kusoma na kuainisha katika vitabu teule vilivyotafsiriwa kutoka kiswahili kwenda kiingereza. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini athari ya uhawilishaji huo kwa ujumbe wa lugha chanzi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha na uhawilishaji huo ukawa na athari kwa ujumbe asilia. Uhawilishaji wa unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa huwa na athari hasi na chanya kwa hadhira lengwa. Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa , uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.