Abstract:
Makala hii imebainisha changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume katika riwaya ya Clara Momanyi; Nguu za Jadi (2021). Katika enzi zetu mwanamke amewekwa mbele kinyume na ilivyokuwa wakati dunia ilikuwa imetawaliwa na ubabedume. Inaonekana kana kwamba mambo yamebadilika. Mabadiliko haya yamemwathiri mwanamume katika jamii. Tafiti nyingi za hapo awali zinaonekana kuegemea zaidi kwenye aina za dhuluma zinazowakumba wanawake katika jamii za Kiafrika. Jambo hili linaathiri jamii kwa kuipa mtazamo kuwa, jinsia ya kiume haikabiliwi na matatizo yoyote. Makala hii iliogozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inatakiwa kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Makala hii itatoa mwanga mkubwa kuhusiana na masuala ya jinsia ya kiume. Aidha, utafiti huu utakuwa kichocheo cha watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume. Halikadhalika, kutokana na makala hii, jamii itaweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili jinsia ya kiume na athari ya changamoto hizo na hivyo itabuni mikakati ya kukabiliana nazo.