Abstract:
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihiwa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia. Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njemaya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Dayiliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalabailiyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Graveiliyotafsiriwa na Githiora (2017). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natalailiyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natalailiyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitileiliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitileiliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skoposna Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadhariaya Skoposiliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duarakutathimini usahihi uhawilishaji huo. Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiriwa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata.Uhawilishaji wa viwakilishivya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera:Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidikufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.