Abstract:
Utafiti huu ulilenga kutathmini Changamoto na Faida za Kufundisha Kiswahili Mkondoni katika Vyuo Vikuu vya Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mawasiliano iliyoasisiwa na wanaisimu Firth, Halliday na Hymes mnamo mwaka wa 1980. Wanaisimu wengine kama vile Naom Chomsky walichangia na kuendeleza nadharia hii. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni mahojiano na ujazaji wa hojaji. Waliotoa taarifa waliteuliwa kimakusudi ili waweze kusaidia katika kupata data iliyohitajika. Wanafunzi wanaosoma somo la Kiswahili wa mwaka wa kwanza, pili, tatu na nne wanaofanya kozi ambazo walimu hutumia teknolojia kufundisha walihusishwa. Hii ni kwa sababu si kozi zote zinazofundishwa mkondoni. Wanafunzi wa uzamifu na uzamili, ambao wanafanya kozi ya Kiswahili, pia walihusishwa. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na kuwasilishwa kwa michemihimili na micheduara. Walimu watano wanaojihusisha na ufundishaji wa Kiswahili mkondoni pia walihusishwa katika kutoa habari.Hii ni kwa sababu wako na tajiriba katika ufundishaji huo.